Kisa cha khidhri by dr hud hud
Khidhri Jina Khidhri hutafsiriwa kwa maana ya “mtu wa kijani” likinasibishwa na neno al-akhdar la Kiarabu lenye maana ya kijani. Katika Hadith, Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, anasema, “Mtu huyu alipewa jina hilo la Khidhri kwa sababu alikaa katika nchi kame, isiyoota kitu, tahamaki ikageuka kuwa ya kijani chini yake.” Rai ya Maulamaa wengi wa Kiislamu ni kwamba Khidhri alikuwa ni Nabii. Qur’an inamzungumzia kama ni mmoja wa waja wa Mwenyezi Mungu waliojaaliwa ilimu, mafuhumu na rehema. “Basi wakamkuta mja miongoni mwa waja Wetu Tuliyempa Rehema kutoka kwetu na Tuliyemuelimisha ilimu zinazotoka Kwetu.” (18:65) Kutokana na Hadith za Mtume Muhammad, swallallahu alayhi wa sallam, ndipo tunapofahamu kwa uhakika kuwa mtu huyo mwenye hikima na ilimu aliyeongozana na Musa na kumfunza mambo mbalimbali alikuwa ni al-Khidhri. Waislamu wanaamini kuwa jamii zote za Mataifa katika vipindi mbalimbali vya historia zilishushiwa nabii mmoja au mwingine...