Uzazi wa mpango
KWA USHAURI MZURI TUMIA TIBA ISIYO NA KEMIKAL
DAWA YA ASILI YA UZAZI WA MPANGO
Kila mtu angependa kuwa na watoto ingawa kila mzazi hupenda apate mtoto kwa wakati muafaka au muda maalumu atakapokuwa tayari kwa ajili ya mtoto. Wakati mtu anapanga kuwa na mtoto ni wakati mzuri sana katika maisha na unatakiwa kuwa ni wakati uliokubalika kwa wazazi wote wawili kuamua kuwa ni kipindi cha kuwa na kulea mtoto
Ili kuepuka mimba zisizotarajiwa wanawake wengi huamua kutumia vidonge vya kuzuia ujauzito (Vidonge vya uzazi wa mpango/majira). Vidonge hivi huwa na madhara mengine mabaya hapo baadaye vikitumika kwa kipindi kirefu.
Zipo dawa za asili kadhaa nyingi zaidi ya 20 ambazo zinaweza kutumika kama njia za kuzuia ujauzito usiotarajiwa bila kukuachia madhara yoyote mabaya. Dawa hizi ama zinazuia urutubishaji wa yai moja kwa moja au huweza kukusababishia kuona siku zako na hivyo kuondoa uwezekano wa kuwa mjamzito.
Nimekuandalia dawa asili nne kwa ajili hii ambazo nimeona zinapatikana kirahisi mazingira ya hapa kwetu Tanzania na ufurahie maisha yako ya ndoa bila kuwa na wasiwasi.
Mhimu: Kama itatokea umepima na kugundulika ni mjamzito basi usizitumie dawa hizi kwani inaweza kupelekea kuharibika kwa huo ujauzito (miscarriage).
Dawa ya asili ya uzazi wa mpango
1. PAPAI
Papai ni dawa bora kabisa ya uzazi wa mpango. Unaweza kula papai mara 2 kwa siku siku 3 hadi 4 baada ya kushiriki tendo la ndoa bila kinga. Litakusaidia kuepuka kutungisha ujauzito. Mbegu za Papai pia ni dawa nzuri ya uzazi wa mpango kwa upande wa wanaume. Zinachofanya mbegu za papai ni kupunguza idadi ya uwingi wa mbegu za mwanaume (sperm count) na ukihitaji kuzaa unaacha tu kuzitumia na hali yako itarudi kama kawaida.
Kula mbegu za papai kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku. Unaweza kuanza zoezi hili wiki 3 kabla hujaamua rasmi kama ndiyo dawa yako ya uzazi wa mpango.
Watu wa bara la Asia wamekuwa wakitumia mbinu hii tangu miaka mingi iliyopita. Dawa hii haina madhara yoyote.
2. TANGAWIZI
Tangawizi huhamasisha kutokea kwa siku zako. Kunywa vikombe viwili vya chai ya tangawizi kila siku ili kuzuia ujauzito. Tumia tangawizi mbichi na siyo ya unga kwa matokeo mazuri zaidi.
3. KOTIMIRI (Parsley):
Kotimiri inapatikana kirahisi Dar Es Salaam na Zanzibar na ni kiungo mhimu kwenye mahoteli mengi ya kitalii. Kunywa kikombe kimoja (robo lita/ml250) asubuhi na jioni cha chai iliyoandaliwa ukitumia kotimiri mbichi kila siku ili kuzuia ujauzito usiotarajiwa. Hakuna madhara yoyote mabaya ya matumizi ya dawa hii.
4. VITAMINI C
Vitamini C ikitumika katika hali yake ya uasili kabisa inaweza kutumika kama dawa ya uzazi wa mpango. Kwenye vitamini C kuna ‘ascorbic acid’ ambayo huzuia homoni inayouandaa mji wa uzazi (‘progesterone hormone’) kushindwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo mimba kukosa mahali pa kukaa baada ya yai kurutubishwa.
Meza viponge vya vitamini C mg 1500 mara mbili kwa siku mbili mpaka tatu baada ushiriki tendo la ndoa bila kinga. Vitamin C ni nzuri pia kwa ngozi yako. Dawa ya asili yenye vitamini C kwa wingi ni unga wa majani ya mlonge. Unga wa majani ya mlonge una vitamini C mara 7 zaidi ya ile ipatikanayo katika machungwa.
Mhimu:
1) Usitumie kiasi kingi sana cha vitamini C kwani inaweza kupelekea mwili wako kutokuwa sawa au unaweza usijisikie vizuri katika mwili wako.
2) Usitumie vitamini C kama unatumia dawa za kuzuia damu kuganda (anti-coagulant medications).
3) Usitumie vitamini C kama una tatizo la sickle cell (sikoseli).
Kumbuka kuwa makini mara zote, na wewe fanya utafiti binafsi pia.
Kama una swali lolote au unahitaji ushauri zaidi niulize ....someni vizuri..ili mupate kuelewa .na kufahamu
Inshaa Allah
Mungu akupe uhai wenye ani ya afya njema
JibuFuta