MAFUTA ya tumbo yanayofanya mtu kuwa na kitambi ambacho hukusanywa kwa njia kuu mbili : Njia ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k SABABU ZA KUPATA KITAMBI Sababu kubwa ya mtu kuwa na kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu (kalori) katika mwili wa mwanadamu, hali inayosababishwa na mtu kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili. VYAKULA VINAVYOCHANGIA KULETA KITAMBI Vyakula vinavyochangia kuleta kitambi ni pamoja na vile vyenye mafuta mengi kama vile nyama nyekundu, nyama ya kuku wa kizungu ( iwe ya kuchemsha, kukaanga ama kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi na jibini), viazi ya kukaanga kwa mafuta maarufu kama chips pamoja na pizza. Vingine ni vyakula vyenye wanga mwingi kama vile ugali wa mahindi uliokobolewa, mihogo, wali, mkate mweupe na vinywaji vyenye sukari nyingi iliyo...
Maoni
Chapisha Maoni