Shairi la tauhid
. *TAUHIIDI NDIO DINI TUSIJE IVUNJA DINI YETU* .. Yuu pwekee yeye mola
Tena hana mshirika
Asie kunywa wala kula
Tena aametukuuka
Hana yeye wa mbadala
Atumikiwa namalaika
*Tauhidi ndio dini tusiivunje diniyeetu*
Ameumba kila kitu
Tena yeye hakuchoka
Zimesimama mbingu bila kitu
Hakuna alozishika
Kaumba majini nao watu
Nawale wa so fahamika
*tauhidi ndio dini tusiivunje dini yetu*
Wana hekima niwaambieni
Tauhiidi tumefunzwa
Tena tusije ua imani
Peponi tuakaja fukuzwa
Tuzidishe zetu imani
Peponi tuje ingizwa
*tauhiidi ndio dini tusiivunje dini yetu*
Hana mshirika mola wetu
Wala yeye hana mfano
Ametukuka mola wetu
Haiitaji mashindano
Tusimshirikishe mola wetu
Tukaja kipata kibano
*tauhiidi ndio dini tusiivunje dini yetu*
Yaa ilahi mola wetu
Bariiki wana hekima
Tufutie makosa yetu
Utujaze nayo hekima
Tukumbatie dini yetu
Tusije iwacha nyuma
*TAUHIIDI NDIO DINI TUSIIJE IVUNJA DINI YETU*
Maoni
Chapisha Maoni